Vilipuzi zaidi ya 15 aina ya ‘explogel 7M V6 watergel explosives’ zimekutwa ndani ya gari la mbunge wa Musoma Mjini anayemaliza muda wake, Vicent Nyerere alipokuwa akifanya mkutano wa kampeni mjini humo.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara, Philip Kalangi, jeshi la Polisi linamhoji mbunge huyo pamoja na dereva na mlinzi wake kufuatia tukio hilo.

Vicent Nyerere

Vicent Nyerere

Alieleza kuwa Nyerere alikuwa anaendelea na mkutano wa kampeni katika eneo la Nyabisari mjini humo ambapo walinzi wake alimfuata na kumueleza kuwa wameona box lenye vitu kama vilipuzi kwenye gari lake.

Kamanda Kalangi alisema kuwa baada ya mbunge huyo kupata taarifa hizo, aliwaagiza walinzi hao kupeleka box hilo jukwaani na ndipo mbunge huyo aliwaonesha wananchi akidai kuwa aliwekewa box hilo na mahasimu wake kwa lengo la kumuua.

Kamanda huyo wa Jeshi la Polisi  Mara aliongeza kuwa waliwaita wataalam wa vilipuzi kutoka Jeshi la Wananchi Tanzania, na walithibitisha kuwa box lile lilikuwa na vilipuzi 15.

“Tunawahoji kwa lengo la kutusaidia kupata taarifa zaidi kwa sababu walituambia kuwa hakuna mtu aliyekuwa anaweza kuingia kwenye gari bila ruhusa, kwahiyo wanaweza kutusaidia kutuambia nani aliweka box hilo ndani ya gari,” alisema Kamanda Kalangi na kuongeza kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa wale watakaobainika kuhusika na tukio hilo.

 

  1. Client’s inputs

Mbowe Aweka wazi Mpango Wa Ukawa Baada Ya Matokeo Kutangazwa
Mourinho: Sijafurahishwa Na Ajira Ya Klopp