Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ureno pamoja na klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo amejumuishwa kwenye orodha ya wachezaji kumi bora ambao bado wanaendelea kutesa kwa kuwa na thamani kubw aya utajiri duniani.

Kwa mujibu wa jariba la Forbes la nchini Marekani, ambalo limekua likitoa orodha ya wanamichezo wenye mkwanja mrefu dunaini pamoja na katika nyanja zingine mara kwa mara, Ronaldo ameonekana kuwa na thamani ya kubwa ya utajiri kutoka uwekezaji wake kibiashara.

Katika orodha hiyo, Ronaldo, yupo katika nafasi ya 8, kwa kuwa na utajiri wenye tahamani ya dola za kimarekani milion 16, ambazo ni sawa na paund million 10.4, huku mcheza gofu anaetamba duniani Tiger Woods akishika namba moja kwa kuwa na utajiri wenye thamani ya paund million 19.5, akifuatiwa na mpinzani wake Phil Mickelson mwenye utajiri wa paund million 18.2.

Mcheza tennes mashuhuri Roger Federer yupo katika nafasi ya tatu kwa kumiliki utajiri wenye thamani ya paund million 17.5, LeBron James ni wa nne kwa kuwa na utajiri wenye thamani ya paund million 17.5.

Mcheza cricket kutoka nchini India Mahendra Singh Dhoni, anashika nafasi ya tano kwa thamani ya paund million 14, mwanariadha Usain Bolt pamoja na Kevin Durant wa klabu ya Oklahoma City ya mchezo wa mpira wa kikapu nchini Marekani NBA, wamefungana katika nafasi ya sita kwa thamani ya paund milion 12.

Nafasi ya saba inashikwa na mchezaji wa gofu Rory McIlroy mwenye utajiri wa thamani ya paund million 8, na nafasi ya kumi ni ipo kwa  Floyd ‘Money’ Mayweather ambaye ana utajiri wenye thamani ya paund milio 7.5.

 

Kampuni ya vifaa vya michezo ya Nike imekamata nafasi ya kwanza kwa kuwa na thamani kubwa ya bidhaa zake upande wa makampuni yanayofanya biashara za kimichezo duniani.

Nike, imebainika kuwa na utajiri wa thamani ya paund billion 17, ikifuatiwa na ESPN yenye paund million 11, huku kampuni ya Adidas ikiwa na thamani ya utajiri wa paund billion 4 na Sky Sports ipo kwenye nafasi ya tano kwa kufikisha thamani billion 3.

Kwa upande wa klabu za michezo duniani, Real Madrid inaongoza kwa upande wa klabu za soka kwa kuwa na thamani ya utajiri wa paund million 301, Manchester United inafuatia kwa kuwa na thamani ya utajiri wa paund million 289, Barcelona ni ya nne kwa kuwa na thamani ya utajiri wa paund million 283 na Bayern Munich ipo kwenye nafasi ya nne kwa thamani ya utajiri wa paund million 243.

Klabu ya American Football ya Super Bowl imeonekana kuongoza kwenye orodha hiyo kwa kuwa na utajiri wenye thamani ya paund million 375 na inayofuata baada ya klabu za soka ni michezo ya Summer Olympics ambayo imeonyesha kuwa na thamani ya utajiri wa paund million 225, na michezo ya Winter Olympics ina utajiri wa thamani ya paund million 185.

Fainali za kombe la dunia zimetajwa kuwa na thamani ya utajiri wa paund million 149 na ligi ya mabingwa barani Ulaya ambayo inaendeshwa na shirikisho la soka barani humo UEFA ina thamani ya utajiri wa paund million 82.

Michezo ya mieleka iliyo chini ya WWE imetajwa kuwa na thamani ya paund million 110.

Magufuli Amvaa Lowassa Dakika Za Mwisho, Atahadharisha
Lowassa kulihutubia Taifa Leo Usiku, Ajihakikishia Ushindi Mkubwa