Cristiano Ronaldo amefanya uzinduzi wa filamu yake ya  iitwayo Ronaldo.

Uzinduzi umefanyika jijini London, England usiku wa kuamkia hii leo na kuhudhuriwa na wageni kibao ila Alex Ferguson ndiye alionekana kuwa mgeni aliyevutia zaidi.

Ronaldo alimkaribisha Ferguson kwa mashamsham ikiwa ni pamoja na kumkumbatia.

Kocha Jose Mourinho aliyewahi kuwa bosi wa Ronaldo pale Real Madrid pia alijitokeza.

Wengine waliohudhuria katika uzinduzi huo ni Radamel Falcao, Carlo Ancelotti, Jorge Mendez, Garry Nevile pamoja na mtangazaji wa michezo wa kutuo wa British Sports TV (Bt Sports) Hayley Mcqueen

Ronaldo aliongozana na mama yake mzazi, maria Dolores pamoja na mtoto wake, Ronaldo Jr.

Filamu hii iliyotengenezwa kwa zaidi ya miezi 14, imeongozwa na muongozaji muingereza Anthony Wonke.

Starring

1.Cristiano Ronaldo

2.Cristiano Ronaldo Jr

3.Maria Dolores Dos Santos Aveiro.

IAAF Yaitega Urusi Hadi Juma Lijalo
Mkurugenzi wa Muhimbili Aandika Historia Kwa Rais Magufuli