Hatimae kocha mkuu wa timu ya taifa ya England, Roy Hodgson ametoboa ukweli wa mambo uliokua unaendelea nyuma ya pazia, baada ya kushindwa kufikia malengo wakati wa fainali za kombe la dunia zilizochezwa nchini Brazil mwaka 2014.

Hodgson, ametoboa ukweli huyo, kufuatia hatua ya chama cha mchezo wa Rugby, kutangaza kumtimua kocha wa timu ya taifa ya mchezo huo Stuart Lancaster, baada ya kushindwa kufanya vyema katika fainali za kombe la dunia la ambazo zilifanyika nchini humo mwezi uliopita.

Hodgson amesema, alikua katika wakati mgumu kama ilivyomtokea Lancaster, lakini busara za baadhi ya maafisa wa FA, zilitumika na kujikuta akinusurika kupoteza kibarua siku chache baada ya kurejea akitokea nchini Brazil, ambapo kikosi chake kiliondolewa katika hatua ya makundi.

Amesema pamoja na kupewa msamaha, aliamuriwa kutimiza masharti ya kuipeleka England kwenye fainali za mataifa ya Ulaya za mwaka 2016, jambo ambalo amelitimiza ipasavyo kwa kikosi chake kufaulu bila kufungwa mchezo hata mmoja katika harakati za kuwania kufuzu.

Lancaster, amelazimika kusitishiwa mkataba wake ndani ya juma hili, hali ambayo ilitarajiwa na wengi kutokana na mashabiki wengi kuonyesha kuchukizwa na uwezo wa timu ya taifa ya England ambayo iliishia kwenye hatua ya makundi.

 

Zlatan Atamba Kulipaisha Soka la Ufaransa
Malinzi Atuma Salamu Za Rambirambi Kwa Musonye