Kiungo wa klabu ya Leicester City, Danny Drinkwater ametajwa katika kikosi cha timu ya taifa ya England, ambacho kitakabiliwa na mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya mabingwa wa dunia, timu ya taifa ya Ujerumani pamoja na Uholanzi juma lijalo.

Drinkwater, ametajwa kwenye kikosi hicho, baada ya kumkuna kocha mkuu wa timu ya taifa ya England, Roy Hodgson ambaye mara kwa mara alionekana akifuatilia michezo ya klabu ya Leicester City, inayoongoza msimamo wa ligi ya nchini humo.

Hodgson checks out Leicester's clash against Liverpool Kocha Roy Hodgson  akifuatilia moja ya michezo ya Leicester City

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 26, amekua muhimili mkubwa katika kusaidia matokeo mazuri kwa klabu yake, hali ambayo ilianza kuhisiwa angeitwa kwenye timu ya taifa, na hii leo imekua kweli.

Kikosi cha timu ya taifa ya England, kisafariki kuelekea mjini Berlin, kupambana na Ujerumani, Machi 26, kabla ya kurejea jijini London katika uwanja wa Wembley kukwaruzana na Uholanzi, Machi 29.

Kikosi cha England kilichotajwa na kocha Roy Hodgson hii leo, tayari kwa michezo hiyo miwili, upande wa walinda mlango ni Jack Butland (Stoke City), Fraser Forster (Southampton), Joe Hart (Manchester City).

Mabeki: Ryan Bertrand (Southampton), Gary Cahill (Chelsea), Nathaniel Clyne (Liverpool), Phil Jagielka (Everton), Danny Rose (Tottenham), Chris Smalling (Manchester United), John Stones (Everton),Kyle Walker (Tottenham).

Viungo: Dele Alli (Tottenham), Ross Barkley (Everton), Eric Dier (Tottenham), Danny Drinkwater (Leicester), Jordan Henderson (Liverpool), Adam Lallana (Liverpool), James Milner (Liverpool), Raheem Sterling (Manchester City).

Washambuliaji: Harry Kane (Tottenham), Daniel Sturridge (Liverpool), Jamie Vardy (Leicester), Theo Walcott (Arsenal), Danny Welbeck (Arsenal).

Mustakabali Wa Yaya Toure Bado Upo Shakani Man City
Audio: Sikiliza hapa wimbo mpya wa Sugu 'Freedom'