Shughuli za kibinadamu zikiwemo ambazo baadhi huwa ni chanzo cha uharibifu wa mazingira kama ukataji miti , uchomaji moto, Kilimo, uchepushaji wa maji na uingizaji wa mifugo kwenye hifadhi umetajwa kuchangia hali mbaya ya sasa ya Wanayama kukosa maji na baadhi ya mito inayotiririsha maji katika mto Ruaha kukauka.

Hayo yamebainishwa na Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi, Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Ruaha, Godwell Ole Meing’ataki na kusema mto huo kwa sasa mto huo hautiririshi maji yake kama ilivyokjwa hapo awali na nia maeneo machache yaliyobaki yenye madimbwi ya maji yanayotumiwa na wanyama.

Hali ilivyo katika Mto Ruaha Mkuu. Picha: Michuzi Jr.

Amesema, uingizaji wa mifugo mingi katika eneo la vyanzo vya maji limekuwa tatizo kuu na shughuli za kilimo holela vimekuwa ni moja ya vyanzo vikuu vya uharibifu na kwamba mabadiliko ya hali ya hewa nayo yamechangia kwa kiasi uwepo wa hali hiyo.

“Kuna uchepushaji mkubwa wa maji katika maeneo mbalimbali ambapo unakuta baadhi ya wananchi wameanzisha mashamba na hawajali kwamba haya maji yanahitajika kwenye matumizi ya maliasili kama hizi za wanyama pori lakini pia kwa ajili ya uzalishaji umeme na matumizi mengine ya kiuchumi,” amesema Kamishna Ole Meing’ataki.

Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi, Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Ruaha, Godwell Ole Meing’ataki akionesha Mto Ruaha Mkuu ulivyokauka. Picha: Michuzi Jr.

Ameongeza kuwa, “Tunafahamu maji yanapojaa kwenye bonde la Usangu hutiririka kupitia Mto Ruaha mkuu na ukipita basi hifadhi tunanufaika kupitia nafasi hii mazingira yatakuwa mazuri na tutapata idadi kubwa ya wageni wanaotembelea hifadhi kwasababu tunarasilimali hii ambayo imehifadhiwa na inategemea huu mto.”

Aidha, Kamishna huyonMsaidizi wa Uhifadhi amefafanua kuwa Upo uwezekano wa madhara ya mto kukauka na hivyo kuathiri shughuli za uhifadhi, maisha ya wanyama wa majini na nchi kavu, na kupoteza watalii ambao huongeza pato la Taifa. 

Rais Samia ampa mwaka mmoja Waziri Makamba

Mbunge atoa tahadhari sheria ulinzi taarifa binafsi
Mashabiki Young Africans washushwa PRESHA