Saa kadhaa zikisalia kabla ya kuanza kwa Mchezo wa Mkondo wa Kwanza Hatua ya Mtoano Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya Club Africain ya Tunisia, Uongozi wa Young Africans unaamini wachezaji watapambana na kupata matokeo.

Young Africans itakua mwenyeji wa mchezo huo utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam kuanzia mishale ya saa kumi jioni, huku ikihitaji ushindi utakaoiweka katika mazingira mazuri kuelekea mchezo wa Mkondo wa Pili.

Afisa Habari wa Young Africans, Ally Kamwe amesema kuwa wachezaji wote wana morali kubwa kuelekea mchezo huo na malengo yao makubwa ni kupata ushindi.

“Wachezaji wamekubaliana kupata ushindi kwenye mchezo wetu wa hapa nyumbani na ule wa ugenini, hivyo mashabiki wasiwe na Presha, wawe pamoja nasi kila hatua kwenye mechi zetu.”

“Ushindani ni mkubwa na tunajua kwamba hakuna ambaye anapenda kuona tunakwama hivyo kila mmoja azidi kuwa pamoja nasi.” amesema Kamwe.

Mshindi wa jumla katika mchezo huo atatinga hatua ya Makundi Kombe la Shirikisho Barani Afrika na kuungana na miamba mingine 15 itakayopata ushindi kwenye hatua hii ya mtoano.

Ruaha Mkuu ‘yalia’ na shughuli za binadamu
Juma Mgunda awapa tano wachezaji Simba SC