Mahakama ya Haki Za Binadamu ya Afrika (AFCHPR) leo inatarajia kuanza kusikiliza kesi ya Nguza Viking maarufu kama Babu Seya na mwanae John Viking maarufu kama Papii Kocha dhidi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kusikilizwa kwa kesi hiyo kunafuatia uamuzi wa Mahakama hiyo kuridhia maombi ya rufani ya wanamuziki hao wenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, uamuzi uliofanywa wiki kadhaa zilizopita.

Hata hivyo, taarifa iliyotolewa na mahakama hiyo, ilieleza kuwa kesi hiyo namba 006/2015 iliyopangwa kusikilizwa Machi 11 haitasikilizwa katika mahakama ya wazi.

Hata hivyo, kwa mujibu wa taarifa za mahakama hiyo, kesi hiyo namba 006/2015 haitasikilizwa katika mahakama ya wazi.

Mahakama ya hiyo ya AFCHPR inaundwa na majaji 11 kutoka nchi mbalimbali na hupokea maombi ya rufani ya kesi ambazo zimemalizika kwa ngazi zote katika nchi mwanachama.

 

 

Marekani yamtumbua Jipu Mtanzania gwiji wa dawa za kulevya duniani
Magufuli apitisha 'fagio' mabilioni ya Benki Kuu