Rais John Magufuli leo amefanya ziara ya kushtukiza katika Benki Kuu ya Tanzania na kuagiza kusitishwa kwa malipo ya malimbikizo ya shilingi bilioni 925.6 yaliyokuwa yameidhinishwa na Wizara ya Fedha.

Rais Magufuli alisitisha malipo hayo na kumtaka Gavana wa Benki Kuu, Profesa Beno Ndulu na Uongozi wa Benki hiyo  kufanya uhakiki wa wafanyakazi wanaopaswa kulipwa fedha hizo kwani kumekuwepo na rundo la wafanyakazi wanaopata malipo pasipokuwa na tija.

4

Alimuagiza Gavana wa Benki hiyo kupitia upya majina ya wafanyakazi wa Benki hiyo ambao ni 1391 na kuwaondoa wafanyakazi ambao hawana ulazima.

“Haiwezekani tukawa na kundi kubwa la wafanyakazi, wanalipwa mishahara wakati hata kazi wanazofanya hazijulikani” Amesema Dkt. Magufuli.

Aidha, alikagua baadhi ya CV za wafanyakazi wa Benki hiyo ili kujiridhisha na uhalali wa uwepo wao katika jengo hilo linalotunza fedha takribani zote za Serikali.

6

Dk. Magufuli aliagiza Kitengo cha Madeni ya nje ambacho awali kilikuwa chini ya Benki Kuu na baadaye kuhamishiwa Wizara ya Feha, kirejeshwe Benki Kuu mara moja ili kuimarisha udhibiti wa ukopaji na ulipaji wa madeni.

Rufaa ya Babu Seya na Mwanae kuanza kutiririka leo Mahakama ya Afrika
Kuibuka Kwa Rashford Na Mkasa Wa Edibily Lunyamila