Ligi Kuu nchini England (EPL) imeruhusu matumizi ya wachezaji watano wa akiba mchezoni badala ya watatu kama ilivyo kwa sasa ili kutoa nafasi kwa makocha kuwapa mapumziko wachezaji.

Mabadiliko hayo yatatumika katika kipindi hiki cha mpito cha janga la virusi vya Corona kwa sababu, timu hazijapata muda wa kujiandaa vizuri baada ya ligi kusimama kwa takribani miezi mitatu huku ikitegemewa kuwa na mechi nyingi za karibu karibu.

Makubaliano hayo yamefikiwa na vilabu vyote vya EPL kupitia kikao kilichofanyika leo Alhamis.

Aidha, kila timu itakuwa na wachezaji tisa wa akiba tofauti na mwanzo ambapo kila timu ilitakiwa kuwa na wachezaji saba pekee wa akiba.

Bodi ya kimataifa inayotunga sheria za kandanda sheria – IFAB walipendekeza kuwepo kwa ongezeko mabadiliko ya wachezaji mpaka watano katika mashindano tofauti tofauti yaliyo rasmi ili vilabu vipitishe hasa kwa kipindi hiki cha ligi kilichosalia.

Ligi Kuu ya England itarudi tena Juni 17 huku mechi kubwa ikiwa ni Manchester City dhidi ya Arsenal mchezo wa kiporo kabla ya ratiba ya kawaida kuendelea Juni 19.

Membe aachwa pekeyake Jahazi za wakosaji CCM, Kinana akiomba radhi
Frank Lampard amnyatia Aubameyang