Rais wa Kenya, William Ruto amempa wajibu mpya Rais wa mstaafu, Uhuru Kenyatta kuwa msimamizi wa mipango ya amani ambayo Kenya imekuwa ikitekeleza katika eneo lote.

Katika hotuba yake, aliyoitoa baada ya kuapishwa kuwa Mkuu wa nchi hiyo, Rais Ruto amedokeza kuwa Kenyatta amefanya kazi ya kupongezwa katika kusimamia mipango ya amani hasa nchini Ethiopia na Ukanda wa Maziwa Makuu.

Amesema, awali alikuwa amemwomba mtangulizi wake Kenyatta kuendelea na kazi hiyo, agizo ambalo yeye Rais Mstaafu Uhuru Kenyata alikubali.

Rais wa Kenya William Ruto (kushoto), akiwa na Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta.

“Kuhusu mipango ya amani katika ukanda wetu ikiwa ni pamoja na Ethiopia na Ukanda wa Maziwa Makuu, nimemuomba kaka yangu Rais Uhuru Kenyatta ambaye amefanya mashirikiano ya kupongezwa na mikoa hiyo na amekubali kuendelea kuongoza majadiliano hayo kwa niaba ya wananchi,” amesema Ruto.

Hata hivyo, Ruto amewahakikishia wakenya kuwa usimamizi wake utaunga mkono mipango ya amani ambayo itaongozwa na Kenyatta.

Aidha ameongeza kuwa, “Nimejitolea kuwa serikali ya Kenya na mimi mwenyewe haswa tutaunga mkono juhudi hizo ambazo zitaongozwa na Rais Uhuru Kenyatta. Na ninataka kuwashukuru kwa kukubali kwa moyo mkunjufu kutuunga mkono na kunisaidia katika afua hizo.”

Kanoute kuikosa Tanzania Prisons, Onyango ndani
Kinda la Tanzania limeanza maisha mapya Barcelona