Rais wa Rwanda, Paul Kagame ametangaza kumfuta kazi katika nafasi ya uwaziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo, balozi Olivier Nduhungirehe kuanzia jana April 9, 2020.

Akitoa tangazo hilo kwa niaba ya rais Kagame, Waziri mkuu wa nchi hiyo amesema sababu za kufukuzwa ni kufanya maamuzi ya serikali kwa kutumia mawazo yake binafsi.

Hayo yamejiri huku wizara ya afya ikitangaza visa vipya vitatu vya wagonjwa wa covid 19 na kufanya idadi ya waathirika katika nchi hiyo kuwa 113.

Waziri wa afya wa nchi hiyo amesema visa hivyo vipya vinahusisha wasafiri wawili kutoka nchi zenye maambukizi na mmoja amepatikana kwenye mtandao wa waliokutana na wagonjwa wa awali.

Imeelezwa kuwa visa hivyo vitatu vimetokana pia na vipimo vya watu 720 ambayo vilikuwa vimechukuliwa kutoka kwa washukiwa wa ugonjwa huo.

CORONA: Southampton kukatwa mshahara
Antonio Nugaz: Uongozi, GSM wametuonyesha njia