Mkuu wa wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma, Bitun Msangi ametangaza kufuta safari za mafunzo za madiwani wa wilaya hiyo na kuwataka wakajifunze vijijini.

Mkuu huyo wa wilaya alitoa tamko hilo juzi alipokuwa akitoa vyeti na tuzo kwa wananchi wa vijiji vya Manhweta, Mseta na Mseta Bondeni katika kata ya Chamkoroma baada ya kufanikiwa katika utunzaji wa mazingira ikiwa ni pamoja na upandaji wa miti na ujenzi wa vyoo.

Alisema kuwa madiwani hao hivi sasa wanatakiwa kutembelea vijiji ili kujionea changamoto zilizoko vijijini na kujadili namna ya kuzitatua.

“Mfano hai ni hapa kwenye kata hii. Kama madiwani wakiamua kuja kujifunza wanaweza wakapata elimu ya kuwaelemisha wananchi wa kata nyingine ambazo usafi wa mazingira bado ni dhaifu,” alisema Msangi.

Matokeo Rasmi ya Uchaguzi wa Arusha Mjini Yatangazwa
Mauaji Burundi Yawakimbiza Wamarekani