Kinara wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga ameonesha nia ya kukubaliana na masharti ya Rais William Ruto juu ya mazungumzo ya Bungeni, kwa kuunga mkono matakwa yake ya awali ya kuundwa kwa timu sawa na ile ya makubaliano ya Kitaifa ya mwaka 2008.
Naibu kiongozi wa chama cha ODM, Wycliffe Oparanya amesema wamemshauri kiongozi wao na hatua hiyo ni muhimu na kwani wanadai haki kama ilivyo katika Mkataba wa Kitaifa, wanapendekeza Ruto na Odinga pia wafanye mazungumzo sawia na kujadiliana kisha kuwasilishwa kwa timu iliyoundwa ili kuchukua hatua.
Viongozi wa Muungano wa Azimio wakiongozwa na Raila Odinga, kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka na kiongozi wa NARC Kenya Martha Karua wakati wa kuteuliwa kwa Kundi la Wabunge wa muungano huo kwa ajili ya mazungumzo ya pande mbili na wenzao wa Kenya Kwanza. Picha ya Wilfred Nyangaresi | Nation Media Group.
Amesema, “ni kwamba jukumu la wakuu wawili katika mazungumzo kutambuliwa. Hawako Bungeni lakini wanapaswa kuwa na njia ambapo wanaweza kufanya kikao na mashauri hayo kuwasilishwa Bungeni ili kuchukuliwa hatua,lakini watu wahusishwe. Hatuwezi kuwaachia wabunge peke yao.”
Alhamisi ya Aprili 6, 2023, Rais Ruto alisema iwapo mazungumzo hayo hayawezi kufanywa Bungeni, Azimio anapaswa kusahau kuhusu mashauriano na serikali akisema, “Hatuwezi kufanya mazungumzo nje ya sheria. Ndio maana nasema tuwaruhusu wabunge wetu wafanye mazungumzo ya pande mbili Bungeni. Ikiwa mazungumzo hayatafanyika Bungeni, basi wao (Azimio) wasubiri 2027.”