Aliyekua meneja wa klabu za Everton na Man Utd zote za England, David William Moyes huenda akarejea tena katika ligi ya nchini humo akiwa na klabu ya Sunderland.

Moyes ambaye alitimkia nchini Hispania, mara baada ya kuondoka Old Trafford mwaka 2014 na kujiunga na klabu ya Real Sociedad, ameripotiwa kuwa katika mazungumo na viongozi wa klabu ya Sundeland.

Mazungumzo baina ya pande hizo mbili yameanza, baada ya kuwepo kwa mpango wa chama cha soka nchini England FA, wa kutaka kumtangaza aliyekua meneja wa klabu ya Sundeland Sam Allardyce kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya nchi hiyo.

Moyes ameonekana kuwa kivutio kikubwa kwa viongozi wa klabu hiyo ya Stadium of Light, kutokana na kuwa uzoefu wa kutosha katika mshike mshike wa ligi kuu ya soka nchini England.

Leonardo Bonucci Ni Chaguo Lingine La Mourinho
Mipango Ya Jurgen Klopp Kumuondoa Joe Allen Anfield