Straika hatari wa TP Mazembe, Mtanzania Mbwana Ally Samatta, ametupia bao mbili wakati timu hiyo ikiitandika El Merreikh ya Sudan na kutoga fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

 

TP Mazembe inatinga fainali hiyo na sasa itaivaa USM Alger ya Algeria na iwapo watashinda, Samatta na Ulimwengu watakuwa Watanzania wa kwanza kucheza fainali hiyo na kubeba kombe.

Fainali hiyo itapigwa Oktoba 30 hadi Novemba Mosi na kurudiwa kati ya Novemba 6 hadi 8.

Mazembe kutoka DRC imetinga fainali kwa ushindi wa jumla wa mabao 4-2 baada ya mchezo wa awali kupoteza mabao 2-1 na bao hilo moja la TP Mazenbe lilifungwa na Mtanzania mwingine, Thomas Ulimwengu.

Samatta amekuwa ndiye mshambulizi tegemeo wa kikosi cha Mazembe.

 

Liverpool Yawawinda Klopp, Ancelotti
Magufuli: Nitaunda Serikali Ya Huduma Za Papo Kwa Papo