Jurgen Klopp na Carlo Ancelotti wamechukua muda mchache kuanza kutajwa na huenda mmoja wao akapewa ajira ya kuwa meneja wa klabu ya Liverpool baada ya Brendan Rodgers kufungashiwa virago jana jioni.

Wawili hao wanazungumzwa sana kuptia vyombo vya habari kwa kuaminika wana uwezo wa kuivusha Liverpool na kuifikisha panapostahili hususan katika msimu huu ambapo mambo yalianza kuonekana kwenda kombo chini ya utawala wa Brensdan Rodgers ambaye tayari mashabiki walikua wameshaanza kuonyesha hawana imani naye.

Uongozi wa Liverpool ulichukua maamuzi ya kumfuta kazi Rodgers mara baada ya mchezo wa ligi kuu ya soka nchini England dhidi ya Everton uliomalizika kwa sare ya bao moja kwa moja.

Juergen Klopp aliyekua akikinoa kikosi cha Borussia Dortmund kabla ya kutangaza kupumzika mwishoni mwa msimu uliopita, na mara kadhaa amekua akionyesha kuwa tayari kurejea katika tasnia hiyo lakini wakati mwingine amekua akisita kufanya maamuzi ya jumla, kwa kisingizio cha kuheshimu maamuzi ya kupumzika aliyoyachukua.

Juma lililopita meneja huyo kutoka nchini Ujerumani alikataa kuajiriwa na chama cha soka nchini Mexico ambacho kinaendelea kumsaka mrithi wa Miguel Herrera, aliyekua kocha mkuu wa timu ya taifa ya nchi hiyo.

Mbali na maamuzi hayo Klopp alishawahi kukanusha taarifa za kuwa mbioni kuajiriwa na klabu ya Liverpool majuma matatu yaliyopita, lakini baadhi ya vyombo vya habari viliripoti yupo tayari kufanya kazi na klabu hiyo kama atapewa nafasi ya kufanya usajili wa wachezaji anaowahitaji.

Kwa upande wa Carlo Ancelotti amkua kimya kwa muda mrefu tangu alipoondoka Real Madrid mwishoni mwa msimu uliopita, na hakuwahi kuzungumza lolote kuhusiana na mustakabali wa shughuli za kiutendaji hususan soka la nchini England.

Hata hivyo bado uongozi wa Liverpool, haujazungumza lolote mpaka sasa, zaidi ya kutoa taarifa za kuachana na Rodgers ambaye aliajiriwa klabuni hapo mwaka 2012 akitokea Swansea City.

Rodgers anandoka Liverpool FC hukua kikumbukwa kwa kufanya usajili wa paund million 80 mwanzoni mwa msimu huu kwa kuwasajili akina Christian Benteke, Danny Ings, Roberto Firmino, Nathaniel Clyne pamoja na Joe Gomez.

Van Gaal Awatafutia Jina Wachezaji Wake
Samatta Atimiza Wajubu Wake TP Mazembe