Nahodha na Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania Mbwana Samatta, amejiunga na Kambi ya timu hiyo nchini Misri, akitokea Ubelgiji anakocheza Soka la kulipwa katika klabu ya KRC Genk.

Samatta amejiunga na kambi ya Stars sambamba na wachezaji wengine wanaocheza soka nchini Ubelgiji Kelvin John (KRC Genk) na Novatus Dismas (Zulte Waregem).

Kundi la pili la Wachezaji wa Taifa Stars lililowasili nchini Misri kujiunga na wenzao kwa maandalizi ya mchezo dhidi ya Uganda

Wakati Samatta na wenzake wakitua kambini Misri, Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Adel Amrouche naye amewasili nchini humo sambamba na wachezaji wa Young Africans ambao walilazimika kubaki Dar es salaam kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya US Monastir.

Taifa Stars itacheza mchezo wa Kundi F, wa kuwania kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika ‘AFCON 2023’ dhidi ya Uganda ‘The Cranes’ Ijumaa (Machi 24) katika Uwanja Suez Canal mjini Ismailia, Misri.   

Uganda wamechagua kutumia Uwanja wa Suez Canal kutokana na viwanja vyao kutokuwa na vigezo vya CAF.

Rais Samia atoa Milioni 878.4 uboreshaji sekta ya mifugo
Ukame kusababisha vifo watu 135 pembe ya Afrika