Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa Umoja wa Afrika (AU), pamoja na Jumuiya za Kimataifa kutatua migogoro inayoendelea katika nchi mbalimbali barani Afrika ili kuipunguzia Tanzania changamoto ya kuwa na idadi kubwa ya Wakimbizi.

Akiwa Addis Ababa nchini Ethiopia kwenye Mkutano wa 33 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa AU, Samia amesema nguvu ya ziada ikiwekezwa kwenye kutatua migogoro hiyo, Viongozi nao watatumia muda mwingi zaidi kwenye harakati za kimaendeleo na hivyo kupunguza Umaskini.

Makamu wa Rais ametaja mapigano na migogoro kuwa ni chanzo kikubwa cha Umaskini katika Bara la Afrika na kusema machafuko yaliyopo yanachelewesha maendeleo.

Mbali na hayo, Makamu wa Rais pia ameuhakikishia Umoja wa Afrika kuwa Tanzania imejipanga kutokomeza kabisa ugonjwa wa Malaria hadi kufikia 2030.

Sumaye arejea CCM, "Mimi sio wa hadhi ya kudharauliwa"
Umoja wa Afrika wakataa mpango wa amani wa Trump