Bondia wa ngumi za kulipwa kutoka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania JWTZ, Seleman Kidunda amewataka mashabiki wake kutulia kuelekea katika pambano lake dhidi ya Eric Mukadi wa DR Congo kwa kuwaambia kuwa kawaida yake kutoa ngumi biriani.

Kidunda ametoa kauli hiyo kuelekea katika pambano hilo linalotarajia kupigwa Juni 30, mwaka huu kwenye Ukumbi wa Mlimani City ambapo Mfaume Mfaume akitarajia kucheza na Nkululeko Mhlongo raia wa Afrika Kusini.

Kidunda amesema kuwa anajua mashabiki wake wamekuwa na kiu ya kumuona ulingoni baada ya kukaa kwa muda mrefu tangu kumalizika kwa pambano lake na Tshimanga Katompa hivyo amewataka watulie kwa kuwa anawaletea ngumi biriani katika pambano lake lijalo dhidi ya Mukadi.

“Najua mashabiki wangu mna hamu kubwa ya kuniona juu ya ulingoni kwa sababu sijapanda ulingoni kwa muda mrefu baada ya kumpiga Katompa kule Songea nataka niwaambie kwamba sina kazi mbovu kaeni tayari kwa kazi kubwa.

“Kawaida yangu kucheza ngumi asali lakini safari hii nawaletea ngumi biryani katika pambano langu la Juni 30, mwaka huu dhidi ya Eric Mukadi yaani atakavyokuja ndivyo nitakavyompokea, nawaomba mjitokeze kwa wingi siku hiyo ili tuliangushe jitu,” amesema Kidunda.

Wanaolazimisha ununuzi Sare, Daftari katika shule zao kukiona
Wasukuma wachekelea huduma Stendi mpya ya Mabasi Nyegezi