Serikali imesema itawadhibu vikali Walimu wakuu walio na tabia na ambao wataendelea kuwalazimisha wazazi kununua sare za wanafunzi kutoka kwenye maduka fulani au ndani ya shule zao zinazouza vifaa ghali.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa hivi karibuni na Katibu katika Wizara ya Elimu nchini Kenya, Belio Kipsang imeeleza kuwa mwenendo huo uliotolewa malalamiko na wazazi ni kinyume cha Sheria ya Elimu ya Kimsingi na kanuni kuhusu Elimu ya Msingi 2015.

Aidha katika kukazia suala hilo, Nakala za barua hiyo zilitumwa kwa walimu wakuu, wakurugenzi wa elimu katika ngazi za kaunti na kaunti ndogo na Afisa Mkuu Mtendaji wa Tume ya Kuajiri Walimu – TSC huku Katibu huyo anayesimamia Idara ya Elimu ya Msingi, akisema wazazi wako huru kununua sare na mahitaji mengine ya wanafunzi kutoka kwa maduka wanayotaka.

Hata hivyo, Dkt Kipsang alisema Sheria ya Elimu ya Msingi, malengo ya elimu bila malipo na kanuni nambari 67 (3) ya Kanuni kuhusu Elimu ya Msingi, 2015, inaweka wazi kuwa hakuna shule ambayo inaruhusiwa kuamua mfanyabiashara au duka ambalo wazazi au walezi wanafaa kuenda kununua sare na vifaa vingine vya shule.

Zimbwe Jr afichua siri ya mafanikio Simba SC
Seleman Kidunda awaahidi mashabiki kitu kizito