Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli amezindua Ndege mpya mbili za Air Tanzania aina ya Bombadier Q400 katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere Dar es salaam.

Rais Magufuli amezindua ndege hizo Leo September 28 2016 ambapo ndege hizo zimenunuliwa na Serikali kwa ajili ya kutumiwa na Shirika la Ndege Tanzania (ATCL)

Katika uzinduzi huo Rais Magufuli amehutubia wananchi waliofika kushuhudia zoezi.  Hizi hapa sentensi 16 katika hotuba yake;

 1. “Waandishi na ninyi mnatumika kuichafua nchi yenu, kwa hiyo tutangulize uzalendo wa nchi yetu” – Rais Magufuli
 2. “Natamani siku moja malaika washuke wazime mitandao yote ili baada ya mwaka wakute tumeshatengeneza TZ mpya, wanapost vingine vya ovyo” – Rais Magufuli
 3. “Ingekuwa ukipewa Urais miaka miwili na nusu unaachia ningefurahi kwa sababu kazi hii ni mateso hulali unafanya kwa ajili ya Watanzania” – Rais Magufuli
 4. “Huyo aliyesema ndege hii haikimbii awe mtu wa kwanza mimi nitamlipia nauli halafu akae mbele akaone mawingu yanavyopiga” – Rais Magufuli
 5. “Wapo waliosema ndege hizi hazitembei ni kama bajaji, hebu fikiria imetokea Canada mpaka Dar es salaam” – Rais Magufuli
 6. “Ndege hizi haZitumiki Tanzania tu, Marekani wanazo 40” – Rais Magufuli
 7. “Niwaombe watanzania tusipuuze vitu vyetu, hata kama hutaki kwa nini usikae kimya” – Rais Magufuli
 8. “Tuna mpango wa kununua ndege zingine 2, moja itakuwa ya kubeba watu 160, nyingine itakuwa inabeba watu zaidi ya 240” – Rais Magufuli
 9. “Tuliamua Serikali tununue moja kwa moja halafu tuwakodishie ATCL ili waache kufanya kazi kwa mazoea” – Rais Magufuli
 10. “Tulipochukua hatua ya kuwashika RAS, DED Kagera leo balozi wa Uingereza ametuchangia Bil 6 kwa ajili ya wananchi Kagera” – Rais Magufuli
 11. “Tuna mpango wa kununua ndege zingine 2, moja itakuwa ya kubeba watu 160, nyingine itakuwa inabeba watu zaidi ya 240” – Rais Magufuli
 12. “Ukitumia ndege za Jet kwenda Songea mafuta ni mil 28.9, lakini ndege hizi mafuta ni milioni 1 kama utaenda Songea” – Rais Magufuli
 13. “ATCL lilikuwa linajiendesha si kiueledi, lilikuwa limebweteka, wafanyakazi wanafanya kazi kimazoea” – Rais Magufuli
 14. “Viongozi, wakurugezi wa ATCL walikuwa wanajilipa 50000 kila wanapotembelea uwanja wa JNIA wakikagua utendaji wa shirika” – Rais Magufuli
 15. “Wengine ndege hizi wamenunua kwa bei kubwa lakini sisi wenye Cash tumenunua kwa bei ya chini” – Rais Magufuli
 16. “Tulianza na kulipa 40% na walipomaliza tulimalizia 60% na tuna mpango wa kununua ndege nyingine 2 kubwa na fedha zipo” – Rais Magufuli

Mambo 3 yanayofelisha maisha
Mama Diamond (Bi Sandra) amtakia Wema Sepetu Happy Birthday