Mkuu wa Mkoa Dodoma, Rosemary Senyamule ameungana na Viongozi wa Dini, Viongozi wa Vyama vya Siasa, Viongozi wa taasisi za Umma, Viongozi wa Serikali, Wabunge, Madiwani, Baraza la wazee , wafanyabiashara ,sekretarieti ya Mkoa, Wakuu wa vyuo, Machifu, wananchi wa Mkoa wa Dodoma na Makundi mbalimbali na kupata iftari ya pamoja aliyoiandaa nyumbani kwake Uzunguni.
Katika iftari hiyo iliyoongozwa na Mgeni Maalimu Mkuu wa Mkoa Arusha ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wakuu wa Mkoa, John Mongela pia ilihudhuriwa na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Sheikh Mustapha Shabaan, pamoja na kulenga kutoa sadaka na kukuza mahusiano mema baina ya wananchi na viongozi katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhan.
Baadhi ya wageni waalikwa walioshiriki katika Iftar ya pamoja iliyoandaliwa na Ofisi ya Mkoa wa Dodoma nyumbani kwake Uzunguni Jijini Dodoma.
Senyamule ametoa salamu za shukurani kwa viongozi mbalimbali wa dini, serikali na wananchi waliofika kwenye iftari hiyo kwa kufanikiwa kujumuika pamoja katika tukio lilalojenga umoja, amani na mshikamano miongoni mwajamii.
“Tuliona kama Mkoa ni nafasi nzuri ya kukaa na nyie pamoja na kula chakula hiki lakini kuwapongeza kwa kazi ambayo mmekuwa mkifanya katika kipindi hichi cha mfungo, najua ukiwauliza watu kwenye mfungo unafanya nini wanasema tunafanya toba kwa Mwenyezi Mungu atupe rehema kwa mambo tuliyo mkosea, maombi maalum kwa ajili ya mambo ambayo tuna yahitaji kama familia, Viongozi na Taifa “Amesema Senyamule.
Hafla hiyo ya iftari imehudhuriwa na Naibu Waziri na Mbunge wa Dodoma mjini, Anthony Mavunde, Wabunge wa Viti maalumu, Wakuu wa Wilaya na Viongozi mbalimbali.