Beki wa pembeni wa mabingwa wa soka nchini Ufaransa PSG  Serge Aurier, amekanusha kufanya mazungumzo na viongozi wa FC Barcelona.

Aurier aliliripotiwa kufanya mazungumzo na mabingwa hao wa soka nchini Hispania kupitia kwa wakala wake, ikiwa ni sehemu ya kutimiza mipango ya kusajiliwa huko Camp Nou.

Taarifa zilieleza kuwa wakala wa beki huyo kutoka Ivory Coast, alizungumza na uongozi wa Barca kabla ya sikuku ya Krismasi mwaka 2016.

“Hakuna ukweli wa jambo hilo, na mimi ninalisikia na kulisoma katika vyombo vya habari. Nimekua mtu mkimya sana, nadhani udhaifu huu ndio unatumiwa na baadhi ya vyombo vya habari kuzusha mambo kama haya,”

“Bado nipo PSG na nitaendelea kuwepo hapa kwa kuheshimu mkataba wangu, na kama litatokea la kutokea kila mmoja atafahamishwa, kwa sababu suala la uhamisho huwa halifanywi kuwa siri.

“Lakini kwa upande mwingine inafurahishwa kusikia ama kuona jina lako linatajwa na kuhusishwa na klabu kubwa kama FC Barcelona, japo ninaendelea kusisitiza sijazungumza na yoyote, wala wakala wangu hajawahi kuonana na viongozi wa FC Barcelona.” Alisema  Serge Aurier

FC Barcelona wapo katika mpango wa kusaka beki wa kulia, baada ya kuondoka kwa Dani Alves aliyejiunga na Juventus mwanzoni mwa msimu huu.

Memphis Depay Mguu Ndani, Mguu Nje
Man Utd, Everton Zamponza Mike Dean