Mwamuzi Mike Dean ameondolewa kwenye orodha ya waamuzi watakaochezesha michezo ya ligi kuu ya nchini England ya mwishoni mwa juma hili.

Uwamuzi wa kumuondoa Dean, umefikiwa na chama cha waamuzi cha England, kufuatia udhaifu mkubwa aliounyesha katika michezo miwili aliyochezesha mwezi Disemba mwaka 2016.

Dean mwenye umri wa miaka 48, alivurunda katika mchezo wa ulioshuhudia Man Utd wakiifunga West Ham Utd ambapo alitoa kadi nyekundu kwa Sofiane Feghouli iliyokuwa na utata, sambamba na kukubali bao la Zlatan Ibrahimovic ambaye alikua amezidi.

Kosa lingine ambalo limemtia hatiani Dean ni kushindwa kumtoa uwanjani kiungo wa Everton, Ross Barkley kufuatia kumchezea rafu mbaya kiungo wa Liverpool, Jordan Henderson.

Wakati Dean akitumikia adhabu ya kuondolewa kwenye orodha ya waamuzi watakaochezesha michezo ya ligi kuu mwishoni juma hili, bado ataonekana katika mchezo wa ligi daraja la kwanza kati ya Leeds United na Barnsley

Serge Aurier: Sijazungumza Na FC Barcelona
Lembeli kuwashtaki mafisadi kwa JPM