Wakati Dunia pikihitimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kwa na maadhimisho ya haki za Binadamu, Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake
Tanzania, Zanzibar – TAMWA ZNZ, kimeiomba Serikali, Asasi za Kiraia na Wadau wote kuimarisha uhuru wa Habari na kufikiwa kwa taarifa.

Katika siku hiyo yenye ujumbe unaosema “Uhuru, Usawa na Haki kwa wote,” pia imetoa nafasi kwa Mataifa kujipima kiwango  cha kutekeleza uhuru huo na kuweka mikakati kwa mwaka 2024, ili kuwa na uimarishaji zaidi.

Taarifa ya TAMWA – ZNZ iliyotolewa na Mkurugenzi wake Dkt. Issa Mzuri imeeleza kuwa, uhuru wa Habari una umuhimu wa pekee ambao utaifanya jamii kuelewa masuala mbalimbali yanayowakabili na kushiriki
kikamilifu katika kuleta suluhisho.

Dkt. Mzuri Issa.

Kwa muda mrefu sasa, Waandishi wa Habari wamekuwa wakihimiza mabadiliko ya sheria za habari ambazo zimepitwa na wakati, hasa Sheria ya Magazeti Na. 5, 1988 iliyofanyiwa marekebisho 1997 na sheria ya Utangazaji Na 7, 1997 iliyofanyiwa marekebisho 2010.

TAMWA – ZNZ inafafanua kuwa, Sheria hizo zikifanyiwa marekebisho vizuri ikiwemo ya kuwalinda Waandishi wa Habari, kuheshimu uhuru wa uhariri, kurahisisha usajili, kuweka bodi inayojitegemea, kuondosha maneno ya ujumla kama “maslahi ya taifa” na kuruhusu Mahakama kuwa ndiyo muamuzi wa mwisho wa makosa basi zitakuwa ni kichocheo cha mijadala na maendeleo ya nchi kiuchumi na kidemokrasia.

Taarifa hiyo inabaishisha kuwa, hali hiyo itakwenda sambamba na ukuwaji wa elimu na teknolojia nchini, kwani Vijana wengi wanasomea uandishi wa habari na kutumia teknolojia kupitia vyombo vya habari vya kawaida na mitandao ya kijamii.

Aidha, taarifa hiyo imeeleza kuwa, wajibu wa kulinda na kuheshimu haki za binadamu ni wa kila kundi ikiwemo jamii, Serikali, vyombo vya Habari na taasisi, hivyo ni vyema kuweka sheria imara zitakazohakikisha haki hizo zinalindwa kila sehemu.

Haki hizo za binadamu zinahusisha pamoja na ile ya kuishi, uhuru wa kujieleza, uhuru wa dini, haki ya kupata elimu, kuwa na maisha bora na yenye hadhi na kinga dhidi ya ubaguzi na unyanyasaji.

Tamko la Haki za Binadamu lilitangazwa rasmi
mwaka 1948 mjini Paris, Ufaransa kwa lengo la kulinda na kuheshimu haki za msingi za kila mtu ikiwemo haki ya kujieleza.

Desemba 10, 1948 Umoja wa Mataifa – UN, ulitangaza Azimio la Haki za Binadamu ambalo nchi zote zinapaswa kuzifuata ili kuharakisha haki za kila binadamu katika nchi.

Miezi 10 tangu afariki: Hatimaye Lokassa ya Mbongou azikwa
Ya Kibwetere: Akili za kuambiwa changanya na zako