Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba, amewaomba watanzania kuendelea kuvumilia suala la tozo za miamala wakati serikali ikipanga kukutana na watoa huduma wa mitandao ya simu juu ya majadiliano ya kupunguza gharama za tozo kwa pande zote mbili.

Ameyasema hayo leo Agosti 20, 2021, wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam, ambapo amesema kuwa licha ya wananchi kutoa malalamiko juu ya ongezeko la tozo lakini bado wameendelea kufanya miamala ya kutuma ama kupokea pesa na serikali tayari imekusanya kiasi cha shilingi bilioni 48.4 kutokana na tozo hizo.

“Tuwaombe wananchi waendelee kuwa wavumilivu tujipe muda tu-engage na wenzetu kwamba, tulivyojumlisha kwetu na nyie huu mzigo umekuwa mkubwa sana kwa wananchi hivi kweli hatuwezi kuangalia nani apunguze wapi, kuna maeneo serikali imeenda kukutana juu kwa juu na watoa huduma na hii si kwa watu wa chini ni kwa watu wanaotuma miamala ya laki 8 au milioni 2, amesema Waziri Nchemba.

Ombi langu moja kwa Watanzania wanaonitizama kwamba jambo hili ni letu sote sio la serikali, nchi hii ni yako wewe hapo ulipo na pesa ni yako na haya mambo tuliyokuwa tunapangilia tuyafanye ni yako, hivyo haya yote ni yetuamesema Waziri Nchemba.

Azam FC yazindua jezi mpya
Tanzania yapokea mkopo wa tilioni 2.7