Waziri wa fedha na mpipango Dkt. Mwigulu Nchemba amepokea mkopo wa shilingi tilioni 2.7 kutoka Benki ya Dunia (WB).

Makabidhiano hayo yamefanywa na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia,  Mara Warwick ndio Wamesaini mikataba hiyo kupitia Shirika la Maendeleo la Kimataifa (IDA).

 Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepokea mkopo huu wenye masharti nafuu utakao tumika kwenye miradi itakayotekelezwa kama vile sekta ya Elimu, Barabara, Tehama na Nishati ya umeme, Tanzania Bara na Zanzibar.


Barabara za vijijini zitanufaika kwa mkopo wa Bilioni 693.2, mazingira ya elimu ya juu wa bilioni 982.1 bilioni na digitali bilioni 346.6.

Aidha,huduma za umeme Zanzibar zitanufaika kwa mkopo wa Bilioni 328.1 bilioni ukiwemo mkopo wa Bilioni 346.6 kwa ajili ya kuboresha maisha ya wananchi visiwani humo.

Serikali kuja na tamko rasmi tozo za miamala
Mbowe majanga hayaishi