Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali itaendelea kutoa ushirikiano kwa taasisi mbalimbali zinazowahudumia mahujaji wanaokwenda Makka, Saudia Arabia kutekeleza ibada ya hijja baada ya kukamilika kwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

Dkt. Mwinyi ameyasema hayo hii leo Aprili 22, 2023 wakati akihutubia Baraza la Eid -El-Fitr kwenye ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdul Wakil, Mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar.

Aidha, Rais Alhaj Dk.Mwinyi amewasihi jamii kuendelea kupiga vita mambo yasiyoendana na maadili, mila ,silka na tamaduni za Wazanzibari ili kupata kizazi kilichoongoka.

Akizungumza suala la maadili wakati wa Sikukuu ya Eid El Fitr, Rais Alhajj Dkt. Mwinyi ameihimiza jamii kuendeleza maadili kwa kujiepusha na vitendo viovu vikiwemo uvunjifu wa amani, udhalilishaji,rushwa , ubadhirifu na dhulma.

Serikali yawatua mzigo wadaiwa pango la Ardhi
Polisi wafukua miili mingine 10, watano familia moja