Serikali nchini, imesema ilipokea mkopo wa masharti nafuu wa dola za kimarekani Bilioni 567.25 sawa na shilingi Trilioni 1, 29.74 kutoka shirika la fedha la kimataifa – IMF chini ya RCF, ili kutekeleza mpango wa kukabiliana na athari za kijamii na kiuchumi zitokanazo na Uviko-19.
Hayo yamebainishwa hii leo Aprili 4, 2023 Jijini Dodoma na Profesa Henry Mollel wakati akitoa taarifa fupi ya ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa mpango wa kukabiliana ma athari hizo za kijamii na kiuchumi.
Amesema, “lengo kuu la mpango huo ni kupunguza athari za kijamii na kiuchumi kutokana na janga la UVIKO-19 Nchini Tanzania, huku akitaja Sekta zilizonufaika na mpango huo ni pamoja na Sekta za Elimu, Utalii, afya, na Maji pamoja na mpango wa kunusuru kaya masikini yaani TASAF.”
Aidha, Prof. Mollel amesema utekelezaji wa TCRP ulihusisha wadau kutoka sekta mbalimbali Wizara ya Fedha na mipango ulioratibiwa na Chuo kikuu cha Mzumbe, kupitia kituo cha umahiri katika ufuatiliaji na tathimini ya mifumo ya Afya.
Hata hivyo, amesema mbinu mbalimbali zilitumika katika kukusanya taarifa ili kufanikisha utekelezaju wa miradi ikiwa ni pamoja na kufanya mikutano na wadau kutoka sekta tano za kipaumbele mapitio ya taarifa za utekelezaji wa kisekta.
“Pia ilihusisha uhakiki wa miradi na kufanya mahojiano na wawakilishi kutoka taasisi za utekelezaji, na ufuatiliaji huu ulifanyika katika mamlaka 184 za Serikali za Mitaa katika Mikoa yote 26,” amesema Mollel.
Taarifa ya ufuatiliaji na tathimini ilibaini baadhi ya miradi kukamilika na ilikuwa katika hatua za mwisho na miradi michache ilikuwa katika hatua za kati na pia ilibainika kuwa rasilimali fedha zilizopokelewa na sekta zote za utekelezaji zilizoelekezwa kwenye utekelezaji wa miradi.