Baraza la kitaifa la muungamo wa wauguzi nchini Kenya – KMPDC, limefanya msako kaunti ya Mombasa na kufunga hospitali 46 zilizokuwa zikiendesha huduma bila vyeti na kwa kutoa huduma za afya chini ya viwango stahiki.
Naibu Afisa Mkuu Mtendaji wa KMPDC, Phillip Meli, amesema zoezi hilo ni endelevu na wale watakaobainika kukiuka vigezo stahiki watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.
Amesema, “haiwezekani kuendelea kuihudumia jamii kwa njia za namna hii, hili jambo haliwezi kuvumilika na wale wote atakaokiuka njia sahihi za kimamlaka watakamatwa watafungiwa huduma na hata kushitakiwa.”
Aidha, ameitaka Serikali ya kaunti ya Mombasa kutoruhusu Hospitali hizo kuendelea kutoa matibabu, hadi pale zitakapohitimu kikamilifu.