Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema amefurahishwa na mafanikio ya utekelezwaji wa ujenzi miradi mbalimbali ya maendeleo yanayoonekana katika maeneo mbalimbali nchini, ikiwemo Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi.

Majaliwa ameyasema hayo, baada ya kukagua ujenzi wa jengo la utawala shule ya Sekondari ya Wasichana Ruangwa (Ruangwa Girls), pamoja na madarasa katika Shule ya Sekondari ya Kitandi iliyopo Wilayani Ruangwa.

Amesema, “Wana-Ruangwa lazima tuendelee kumshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuidhinisha fedha nyingi za utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo. Haya ni mafanikio makubwa, Ruangwa kwa maendeleo inawezekana.”

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipokuwa akizungumza na akina mama waliokuwa wakipata huduma za matibabu ya watoto wao katika Kituo cha Afya cha Narungombe wilayani RuangwaNovemba 18, 2022.

Aidha, Waziri Mkuu pia amesema Rais Dkt. Samia anaridhia kutoa fedha kwa ajili ya kujenga miundombinu mbalimbali ya utoaji huduma za jamii hapa nchini hivyo ni jukumu la kila wananchi ni kuitunza ili ilete faida anayoikusudia

Aidha, ametumia fursa hiyo pia kutoa wito kwa wanafunzi kujitahidi kufanya vizuri kwenye masomo yao akisema, “Rais Dkt. Samia ameweka mkazo katika elimu, ambayo inatolewa bure kuanzia awali hadi kidato cha sita jitahidini katika masomo.”

Dube afichua siri ya kuiadhibu Simba SC
Waziri atoa maagizo kwa kamati za ulinzi na usalama NEMC