Rais wa jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dokta John Magufuli amewataka walimu kupuuza taarifa inayoeleza kuwa serikali imefuta mafunzo ya ualimu wa shule za msingi na awali kwa ngazi ya cheti na kuwa mafunzo yataanzia diploma.

Leo tarehe 5 Oktoba, katika Kongamano la Kuadhimisha Siku ya Walimu Duniani lililoandaliwa na CWT, Dodoma, Rais John Pombe Magufuli alipiga simu ‘live’ na kuongea na washiriki wa kongamano na pia kukanusha kufutwa kwa ualimu wa ngazi ya cheti.

Rais Magufuli amewataka walimu kupuuza taarifa hiyo na kusema kuwa tangazo hilo ni la kipumbavu na kwamba ataendelea kuwa pamoja na walimu wote

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Oktoba 6, 2020
Papa Francis ataka utaratibu mpya wa ulimwengu