Serikali imepanga kuzalisha mitamba zaidi ya milioni 1 kwa mwaka ili kukuza sekta ya mifugo hapa nchini na kuchochea ujenzi wa uchumi wa viwanda.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina ambapo amesema kuwa Serikali imejipanga kuhakikisha kuwa sekta hiyo inatoa mchango mkubwa katika ujenzi wa uchumi na ustawi wa wananchi.
“Vituo vya uzalishaji vilivyopo Arusha na Sao Hill Iringa vimeboreshwa ili viweze kutoa mbegu bora za kutosha kwa kufanya maboresho makubwa katika vituo vya kanda vya uzalishaji mbegu za mifugo,” amesema Mpina
Amesema kuwa kuelekea uchumi wa viwanda, Serikali imejipanga kuzalisha mifugo mingi ya kutosha ili kupata bidhaa bora zitokanazo na mifugo.
Aidha, ameongeza kuwa Serikali imevunja mikataba na wawekezaji wengi ambao hawakuweza kutimiza malengo ya uwekezaji katika sekta ya mifugo.
-
Hofu yatanda kundi la paka kushiriki mazishi Lindi
-
Afisa Elimu, Mkuu wa shule kibeta wasimamishwa kazi
-
JPM ahoji ubaya wake upo wapi, awakumbusha haya wafanyakazi
Hata hivyo, katika kuboresha sekta ya uvuvi Waziri Mpina amesema wafanyabiashara watumie fursa ya kuzalisha nyavu halali ili kuchochea ukuaji wa sekta ya uvuvi kwa kuwa kuna mahitaji makubwa ya bidhaa za uvuvi.