Mikoa ya Lindi na Mtwara itaondokana na hali ya kukatika umeme mara kwa mara katika maeneo ya Mikoa hiyo inayotokana na ubovu wa Genereta moja kati ya Tisa katika kituo cha kuzalisha umeme kwa kutumia Gesi Asilia Mtwara.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Newala Mjini, Kapteni Mstaafu George Mkuchika alilouliza kuhusu umeme wa uhakika na wa kutosha baada ya kugundulika kwa Gesi lakini bado kumekuwa na tatizo la kukatika kwa umeme.

Dkt. Kalemani amesema kuwa katika kuondokana na tatizo hilo Serikali inafanya ukarabati wa Mtambo ulioharibika ili kurudisha uwezo wa kituo katika hali yake ya kawaida ya kuzalisha MW 18.

“ Nia ya Serikali ni kuhakikisha wananchi wake wanapata huduma ya Umeme kwa asilimia kubwa hasa kwa wale waishio vijijini” amesema Dkt. Kalemani.

Aidha, ameongeza kuwa katika kuendeleza juhudi za upatikanaji wa umeme katika mikoa ya Lindi na Mtwara imeongezewa mitambo sita (6) yenye uwezo wa kuzalisha umeme wa jumla ya MW 12 kama hatua ya muda mfupi.

Hata hivyo, amesema kuwa katika kuboresha hali ya upatikanaji endelevu wa umeme katika Mikoa hiyo, TANESCO inajenga njia ya kusafirishia umeme yenye msongo wa kilovoti 132 yenye urefu wa kilomita 80 kutoka Mtwara hadi Mnazi mmoja Lindiuio

Mkulima Market kuandaa soko la wazi Jijini Dar
Serikali kutatua kero ya maji Chalinze