Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima ameagiza jengo la huduma za mama na mtoto katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekou-Toure kukamilika na kuanza kutoa huduma kabla ya Disemba 31, mwaka huu ili wananchi waanze kunufaika.

Ametoa maagizo hayo wakati wa ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya katika shughuli za Maendeleo ya Jamii, mkoani Mwanza ikiwa ni mwendelezo wa ziara zake iliyoanza Mkoa wa Mara.

“Hapa tulipo bajeti ilikuwa ni Bion 10 na kitu, zimeshatoka Bilion 9 bila matatizo kabisa, na sasa zimebaki Bilion 6 ambazo zimepitishwa kwenye Bajeti hii ya Serikali ya awamu ya 6 ya mwaka 2021-2022, na hizo hela zinatakiwa kuanza kutumika ili zitutoe kwenye asilimia 83 twende kwenye asilimia 100 kabla ya kumaliza tarehe 31 Disemba vitoto vile vitavyozaliwa vizaliwe humu ndani,” Amesema Dkt. Gwajima.

Aidha, Dkt. Gwajima amesema kuwa ili kuendelea kuishi kwa afya njema na kushuhudia maendeleo yanayofanywa na Serikali, ni muhimu kwa wananchi kujikinga na maradhi ikiwemo kupata chanjo ya kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa Corona, huku akisisitiza kuwa hata katika nchi za Ulaya wengi waliofariki na ugonjwa huo unaoepukika wengi ni waliokataa kuchanja.

“Usipochanja utapata maambukizi ya ugonjwa wa Corona, na kuwa kwenye nafasi kubwa ya kupoteza maisha, kama wanavyokufa kwenye nchi nyingine zote za Ulaya ambao wamekataa kuchanja” amesema Dkt. Gwajima.

Gor Mahia kumsajili Francis Kahata
Gomes uso kwa macho na Sven Vandebroeck