Serikali imetangaza kuzifutia mbali meli mbili za Tanzania zilizokamatwa zikisafirisha dawa za kulevya na silaha na kusema kuwa Tanzania haiusiki na meli hizo zilizokamatwa zikipeperusha bendera ya Tanzania.

Meli hizo zilikamatwa Disema, 2017 zenye namba za usajili IMO 6828753 imekutwa na kilo 1600 za dawa za kulevya kutoka Jamhuri ya Dominika, na nyingine yenye namba IMO 7614966 imekamatwa ikiwa na silaha zilizokuwa zikisafirishwa kwenda Libya kinyume na sheria za kimataifa.

Taarifa hiyo imetolewa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu, na kusema kwamba meli hizo zilisajiliwa chini ya mamlaka ya usajili wa usafiri wa baharini, lakini hata hivyo zilishasajiliwa kinyume na sheria.

“Tanzania haihusiki na shehena za silaha wala mdawa ya kulevya yaliyokamatwa ndani ya meli hizo, bali ilitoa usajili wa meli hizo chini ya mamlaka za usajili ambao ni utaratibu wa kawaida wa kimataifa wa kusajili meli duniani, kwa hiyo kufuatia tukio hilo, tumezifutia usajili meli zote mbili, usajili ulitolewa chini ya taasisi ambayo ilishanyimwa kibali cha kusajili meli, na sasa meli zote zimeshusha bendera ya Tanzania ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa”, amesema Mama Samia Suluhu

Sambamba na hilo serikali imesema kuanzia sasa mamlaka husika inapitia taarifa za meli zote zilizosajiliwa nchini ili kuhakiki taarifa zake, na kutoa mapendekezo ya ushauri kwa serikali.

 

Korea kaskazini na kusini kuishangaza dunia
Rais atoa tamko kuhusu hatma ya uchaguzi Zimbabwe