Takriban watoto 14 wameuawa na wengine kadhaa wamejeruhiwa katika shambulio lililotokea Julai 23, 2022 magharibi mwa Idlib kaskazini mashariki mwa nchi ya Syria.

Taarifa hiyo imetolewa kwa vyombo vya habari na mwakilishi mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto katika ukanda wa mashariki ya kati na kaskazini mwa Afrika Amman, Syria Adele Khodr ambaye amesema UNICEF inalaani shambulio hilo.

Khodr amesema, “tukio hili ni ukumbusho wa kuhuzunisha kwamba vita dhidiya Watoto havijaisha. Watoto wa kaskazini magharibi mwa Syria na kote nchini wanaendelea kulipa gharama kubwa zaidi ya ghasia zinazoendelea.”

Mji wa Idlib uliopo kaskazini mashariki mwa nchi ya Syria.

Mwakilishi huyo wa UNICEF, amekumbusha pande zote zilizo kwenye mzozo nchini humo kuwa Watoto hawapaswi kulengwa kamwe kwenye mapigano kuwa Watoto wanapaswa kulindwa wakati wote na popote walipo na kwamba wanastahili kuishi bila ghasia au woga.

UNICEF imesema, mwaka 2017 asilimia 70 ya ukiukaji mkubwa dhidi ya wato nchini Syria ambao ulitendeka kaskazini magharibi mwa nchi hiyo ulirekodiwa.

Serikali yakataa vifo, uharibifu mali za raia
Mapigano DRC yasababisha vifo vya watu 800