Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi kuacha tabia ya kuharibu miundombinu ya barabara, ambayo imetengenezwa kwa gharama kubwa na serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo.

Rais Samia ameyasema hayo Jijini Arusha wakati akihutubia wananchi katika ufunguzi wa barabara ya Afrika Mashariki (Arusha Bypass) yenye urefu wa kilomita 42.4.

“Niwaombe sana ndugu zangu kufuata taratibu zilizowekwa ili tuendelee kutunza miundombinu yetu, iendelee kutukuzia uchumi wetu,” amesema Rais Samia.

“Kumeanza kujitokeza vitendo viovu vya kuharibu miundombinu yetu tumekuwa tunaoana Jeshi la Polisi wakizungumzia Jinsi ya kutunza barabara zetu kutotengeneza magari ambayo ni mabovu barabarani wanapofanya hivyo wanamwaga mafuta ambayo yanakwenda kutoboa barabara, tufuate masharti yote tunayoambiawa ili kutunza maeneo yetu,” ameongeza.

Rais Samia amesema Swala la kuzidisha uzito kwenye magari ni sababu nyingine ya kuharibu miundombinu ya barabara na uharibifu wa mazingira kama kutupa takataka kwenye madaraja.

“vitendo vingine ni vile vinavyoleta uharibifu kwenye madaraja na kuharibu mazingira nayo ni kutupa taka kwenye madaraja lakini pia kuchimba mchanga, kwenda kuharibu muundombinu huo ni hasara kwa taifa,” amesema Rais Samia.

Aidha amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki zoezi la Sensa ya watu ana makazi itakayofanyika Agosti 23, 2022

Walioghushi fidia ya ardhi 'Airport Dodoma' wabanwa
Mohamed Ouattara atua Misri