Klabu ya Simba SC leo Ijumaa (Julai 22) imeendelea na zoezi la kutambulisha wachezaji waliosajiliwa klabuni hapo kuelekea msimu mpya wa 2022/23.

Simba SC kwa siku kadhaa ilikua kimya katika usajili na kutambulisha waliosajiliwa kwenye kikosi chao, baada ya kufanya hivyo kwa mara ya mwisho kwa Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Ghana Augustine Okrah.

Beki kutoka Ivory Coast Mohamed Ouattara ametambulishwa rasmi kuwa Beki wa kikosi cha Klabu ya Simba SC akichukua nafasi ya Pascal Wawa aliyeondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu uliopita.

Simba SC imemtambulisha Beki huyo kupitia Simba APP na kurasa zake za mitandao ya Kijamii, huku ikiweka video maalum ambayo imethibitisha Ouattara tayari ameshatua nchini Misri kwa ajili ya kuanza maandalizi na wachezaji wenzake.

Video ya utambulisho ya Ouattara imeonesha akiwa Jangwani akiokota jezi ya klabu ya Simba SC ambayo ataitumikia kwa msimu ujao.

Ujumbe wa Simba SC ulioandikwa kwenye kurasa za mitandao ya kijamii kwa ajili ya kumtambulisha Ouattara unasomeka hivi: Beki kisiki, beki wa kuzuia mipira ya juu na chini, beki bora na mwenye uwezo wa kucheza kwenye kikosi chetu. Mohamed Ouattara ni ?????? ?

@ouatt_momoo #Outtara #NguvuMoja

Ujio wa beki huyo umechagizwa na uwepo wa Kocha Zoran Maki, ambaye aliwahi kufanya naye kazi katika klabu za Wydad Casablanca ya Morocco na Al Hilal ya Sudan

Simba SC imefikisha idadi ya wachezaji wanne wa kimataifa waliosajiliwa katika dirisha hili la usajili, wakitanguliwa na Moses Phiri (Zambia), Victor Akpan (Nigeria) na Augustine Okrah (Ghana), huku wachezaji wazawa waliotua klabuni hapo ni Habib Kyombo na Nassoro Kapama.

Rais Samia akemea uharibifu wa barabara
Wakuu EAC wasisitiza umuhimu wa soko la pamoja