Serikali imetoa maelekezo yatayosaidia kudhibiti ajali za barabarani nchini huku ikidai kuroridhishwa na takwimu za ajali barabarani zilizotokea hivi karibuni.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini amesema Serikali ambayo inadhamana ya kulinda usalama wa raia na mali zao isingependa kuona matukio ya vifo na uharibifu wa mali za raia yakiendelea.

“Serikali ambayo ina dhamana ya kulinda Usalama wa Raia na mali zao isingependa kuona matukio ya vifo na uharibifu wa mali za raia wake yakiendelea,” amesema Naibu Waziri.

Ajali ya barabarani

Sagini ameongeza kuwa, “tumemsikia mara kadhaa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akikemea na kulitaka Jeshi la Polisi kuchukua hatua madhubuti kudhibiti ajali za barabarani.”

Kuhusu shida ya usafiri katika baadhi ya maeneo nchini, Naibu Waziri amewaomba watu wenye uwezo na wafanyabiashara kuomba leseni za usafirishaji ili kupunguza adha ya usafiri katika maeneo yenye uhitaji hasa Mikoa ya Simiyu, Kagera, Kigoma, Mara na Geita.

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Sagini amealiagiza Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani kuchukua hatua kwa askari Polisi nchini watakaobainika wanamiliki magari madogo ya abiria ambayo yamekuwa yakilalamikiwa kusababisha ajali.

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Wilbroad Mutafungwa.

Hata hivyo, ameipongeza Kamati ya Usalama kupitia Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, David Kafulila kwa kuchukua hatua za kudhibiti matumizi ya magari ya usafirishaji yaliyosajiliwa yanayokukiuka Sheria kwa kubeba abiria wengi na kwa masafa marefu.

Mkurugenzi Mkuu wa LATRA, CPA Habibu J. Suluo.

Uchaguzi Mkuu Kenya: Tuhuma za utata kwa IEBC
Shambulio lauwa Watoto 14