Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amewasili mkoani Tabora ambapo kesho Novemba 19, 2023 atashiriki katika Sherehe za kumpongeza Mhasham Askofu Mkuu Mstaafu, Paul R. Ruzoka na kumtakia Matashi mema Askofu Mkuu Mpya wa Tabora,  Mwadhama Protase Kardinali Rugambwa.

Sherehe hizo, zitafanyika katika Jimbo Kuu  Kanisa Katoliki Tabora na mara baada ya kuwasili Mkoani Tabora, Dkt. Biteko alipokelewa na Viongozi wa Serikali na Chama cha Mapinduzi, wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Dkt. Batilda Burian.

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Novemba 19, 2023
NSSF yapongezwa matumizi ya TEHAMA Daraja la Nyerere