Wakuu wa Wilaya watatu walioteuliwa hivi karibuni na Rais wa Jamhurii ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kushika wadhifa huo katika Mkoa wa Geita wameapishwa rasmi hii leo na Mkuu wa Mkoa huo Martin Shigela.

Mbele ya Mkuu huyo wa Mkoa, Wakuu hao wapya wa wilaya waliopa ni pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Nyang’hwale, Grace Kingalame ambaye kabla ya uteuzi huo alikuwa mtumishi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).

Wakuu hao wapya wa Wilaya wakila kiapo cha ahadi na uadilifu.

Wengine walioapishwa na Mkuu wa Mkoa Shigela ni Mkuu wa Wilaya ya Geita, Colnel Magembe na Mkuu wa Wilaya ya Chato, Deusdedith Katwale.

Aidha, mara baada ya kuapishwa Wakuu hao wa Wilaya pia wamekula kiapo cha ahadi na uadilifu tayari kwa kuanza kuyatumikia majukumu yao mapya.

Morocco, Iraq wafungua ubalozi baada ya miaka 18
Zoezi uhamiaji Msovera limelinda haki za Binadamu: Serikali