Shilole amesema kuwa aliwahi kukutana na ushawishi wa utajiri kutoka kwa wauza madawa ya kulevya wakimtaka asaidie kusafirisha ‘unga’ huo kupitia safari zake za Ughaibuni.

Hata hivyo, Shishi ameeleza kuwa aliamua kuzitosa ofa zote zilizowekwa mezani na ‘madon wa unga’ kwa kuwa alijua tamaa fedha za haraka haraka zingeharibu muendelezo wa maishayake.

“Kiukweli ushawishi upo niache kusema uongo lakini kwa sababu binafsi na akili zangu timamu na najua nini nafanya basi huwa naweka tamaa pembeni na kuangalia kitu ambacho kina mwendelezo na maisha yangu,” Shilole aliiambia EATV.

Shilole na Nuh Mziwanda

Alisema kuwa alipowakumbuka watu anaowapenda wakiwemo watoto wake pamoja na mpenzi wake Nuh Mziwanda, aliamua kutothubutu kuchotwa na ushawishi huo.

Robert Lewandowski Atoa Siri Ya Mafanikio Yake
Maalim Seif: Msikubali Kuchokozwa