Mwanamuziki Ali Kiba kwa mara ya kwanza ametolea ufafanuzi wa kina chanzo cha kutokea tatizo la kimaelewano kati yake na mmoja wa watu wake wa karibu, Muigizaji na mjasiriamali Esha Buheti, ambaye alizua sintofahamu Muda mfupi baada ya uzinduzi wa Album yake mpya ‘Only One King’ baada ya kuandika ujumbe kwenye ukurasa wake wa mtandao wa instagram, ujumbe wenye kuashiria kujiondoa karibu na Ali Kiba

Esha aliandika hivyo kutokana na kujiona hathaminiki licha ya kujitolea kuwa sehemu ya karibu ya familia ya msanii huyo mahiri wa muziki Nchini, kwa kile kinachodaiwa kuwa Ali Kiba ni kama hamjali na siku hiyo hakumtambua na kama alimyima nafasi ya kuzungumza kwenye hafla ya kuiskiliza album hiyo na badala yake kupewa nafasi hiyo hasimu wake ambaye ni Shilole.

Sasa Kupitia kwenye kipindi cha XXL kinachorushwa kupitia Clouds Fm alikiba amefunguka wazi kuhusu sakata hilo na namna alivyopokea ujumbe mzito wa Esha Buheti wenye kuelezea wazi kuwa ameamua kujiweka pembeni na haoni haja ya kuendelea kujipendekeza kwa kuwa hathaminiwi.

 “kuna vitu ambayo vinaharibu sana watu haya mambo ya social Media, watu wanataka credit sana.

Dada yangu @esha.s.buheti kwa sababu amekuwa kwenye vitu vyangu vingi na nimekuwa nikizungumza naye vitu vingi iwe cha kishenzi au kistaarabu lakini amenistaajabisha sana kwa sababu hajaona thamani niliyompa ya kumuweka karibu na familia yangu, nasikitika sana, Esha sio shabiki wangu ni familia yangu.

Ana connection na familia yangu mama na mke wangu, huwa anakuja nyumbani mara kwa mara. Furaha yangu ya kufanya jambo langu pale Serena watu wengi wameitikia.

Na ile furaha yangu na jambo limekwenda vizuri siwezi kukumbuka kila mtu nilimsahau hadi Aidan Charlie meneja wangu” Alisema Ali Kiba.

Pamoja hayo Ali Kiba ameikanusha dhana iliyopo  kuwa pengine alimpendelea Shilole anayedaiwa kupewa nafasi ambayo ilitakiwa apewe  Esha buheti.

“Kama kuna mtu ana bifu naye alialikwa mimi sikumwalika huyo mtu. Sikumwalika @officialshilole nilistukia tu yupo pale ukumbini na nisingeweza kumkumbuka Shilole kwa sababu sina mazoea naye. Esha namkumbuka sana. Hata unilazimishe vipi nisingeweza kumkumbuka Shilole hatupo karibu kabisa”  aliongeza Ali Kiba.

Mjumbe Maalum UN awakingia kifua Zimbambwe
Kampuni ya Facebook yabadilishwa jina