Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa masuala yanayohusiana na vikwazo Alena Douhan ameiomba Marekani kuondoa vikwazo dhidi ya Zimbabwe ambavyo vimeongeza janga la kibinadamu pamoja na kushuka kwa uchumi. 

Alena amekaa nchini Zimbabwe kwa karibu wiki mbili sasa wakati akitathmini athari zitokanazo na vikwazo vya Marekani kwenye taifa hilo la kusini mwa Afrika.

Marekani imeweka vikwazo vya kifedha na vya kusafiri kwa baadhi ya viongozi wa kisiasa na kijeshi pamoja na wafanyabiashara yakiwemo makampuni yanayohusishwa na serikali, takriban miongo miwili iliyopita.

Ubalozi wa Marekani mapema wiki hii umesema kwamba unaweza kuondoa vikwazo hivyo baada ya kuthibitisha kwamba watu waliowekewa wameacha kuhujumu demokrasia, kushiriki ufisadi pamoja kukiuka haki za kibinadamu.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AP hatua hiyo imechukuliwa baada ya wakulima wa kizungu kupokonywa mashamba yao pamoja na wizi wa kura na ukiukaji wa haki za binadamu kutoka kwa kiongozi wa muda mrefu marehemu Robert Mugabe.

Museveni akana ugaidi Uganda
Sikumualika Shilole/Esha ni ndugu yangu:Ali Kiba