Uongozi wa simba SC umethibitisha Rasmi kuwa kwenye mchakato wa kumuajiri Mkurugenzi wa Ufundi wa Klabu hiyo, iliyoweka malengo ya kuendelea kufanya vizuri Kimataifa.

Simba SC imekua ikihusishwa na mpango wa kuwa katika mazungumzo na aliyewahi kuwa Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Ghana ‘Black Stars’ Kwesi Apiah, ambaye anatajwa huenda akatua Msimbazi kwa ajili ya kushughuli za kiufundi.

Meneja wa Habari na Mawasilino wa Simba SC Ahmed Ally amesema Uongozi upo katika mchakato mzito wa kumsaka Mkurugenzi wa Ufundi ambaye atafanya kazi kwa ukaribu na Benchi la Ufundi la Klabu hiyo.

“Viongozi wa juu Simba SC wanashughilikia mchakato wa kupata Mkurugenzi wa Michezo klabuni kwetu, itasaidia kupunguza Majuku kwa CEO na kwa vile tunataka kuchukuwa Kimataifa lazima tuishi Levo za Kimataifa”

“Wakati wowote Simba SC itampata na kumtangaza Mkurugenzi wa Ufundi, tunaamini anakuja kufanya kazi kubwa ambayo itaiwezesha klabu yetu kuwa katika kiwango kikubwa kiutendaji ndani na nje ya Uwanja.” amesema Ahmed Ally

Simba SC haijawahi kuwa na Mkurugenzio wa Ufundi tangu nafasi hiyo ilipotangazwa na kuingizwa katika katiba za nchi Wanachama wa Shirikisho la Soka Duniani ‘FIFA’ na lile la Afrika ‘CAF’.

TFF kumtangaza kocha mpya Taifa Stars
Wananchi waomba usalama kwa Rais