Mtendaji mkuu wa Klabu ya Simba, Senzo Mazingisa Mbatha amekanusha taarifa zinazoripotiwa Tanzania na Afrika kusini kuwa Klabu ya Simba ina mpango wa kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Zambia na Klabu ya Orlando Pirates, Justin Shonga.

Senzo amesema “Shonga ni mchezaji mzuri sana, kwa sasa hatumhitaji tuna wachezaji wengine wazuri kwenye nafasi anayocheza labda wachezaji hao waondoke ndio tunaweza kumsajili” Pia amesema anaweza akiongezea Simba gharama ambazo sio za Lazima.

Shonga mwenye umri wa miaka 23 ambaye pia anawaniwa na Young Africans mpaka Sasa amecheza mechi 11 za Orlando Pirates bila kufunga goli. Nyota huyo amecheza jumla ya mechi 77 ndani ya Orlando Pirates amefanikiwa kufunga magoli 16 na kutoa Assists 16.

Ibrahim Ajib apewa masharti Simba SC
Dkt. Shein aweka udongo jiwe la msingi ujenzi Ikulu Dodoma