Kocha mkuu wa timu ya Tanzania kwa vijana wasiozidi umri wa miaka 23 Kim Poulsen ameeleza kuwa alipanga kuwaita wachezaji wa Young Africans, Feisal Salum na Dickson Job kikosini kwake lakini imeshindikana kutokana na nyota hao kuwa na ratiba ngumu.

Poulsen alitaja kikisi cha U23 jana Ijumaa (Julai 16), tayati kwa michuano ya Ukanda wa Afrika Mashariki na kati *CECAFA* itakayoanza Julai 18 nchini Ethiopia.

Kocha huyo kutoka Denmark amesema angependezwa kuwa na wachezaji hao wa Young Africans kutokana na uzoefu wao wa kupambana,  lakini hana budi kuheshimu ratiba ya klabu yao.

“Nilipanga kuwajumuisha Feisal na Job, lakini wanakabiliwa na mchezo wa fainali hivyo nimewaacha na nimechagua wengine ambao naamini wataiwakilisha nchi vyema,” amesema Kim.

Sambamba na hao kocha Kim alimuhitaji kipa wa Mwadui Mussa Mbissa, kwenye kikosi chake lakini imeshindikana kutokana na kuchelewa kwa upatikanaji wa baadhi ya nyaraka zake za kusafiria ikiwemo ‘Visa’ hivyo kumuita Daniel Mgore wa Biashara United.

Kwa nini Niyonzima na sio wengine? Ufafanuzi watolewa
Bocco: Tukipongezwa na Mashabiki tunaumia