Nahodha na Mshambuliaji wa Klabu Bingwa Tanzania Bara Simba SC John Raphael Bocco, amesema jambo kubwa linaloumiza klabuni hapo kwa wachezaji wote ni pale wanapopoteza mchezo kisha Mashabiki na Wanachama wakawapigia Makofi.

Bocco amefuchua siri hiyo ya Maumivu kwa wachezaji wote wa Simba SC, alipozungumza na Clouds FM kupitia kipindi cha Sports Extra.

Bocco amesema mazingira ya kupoteza mchezo kwa hakika yanaumiza, hasa kwa wachezaji wanaopambana uwanjani, lakini kwa Mashabiki na Wanachama huumiza zaidi, lakini hushangazwa kuona bado kuna hali ya kupongezwa kwa kupigiwa makofi.

“Kupoteza mchezo ndani ya Simba SC kunaumiza sana, tunaumiaga sana na kinacholeta mtihani ni pale unapoona mmepoteza mchezo lakini Mashabiki wanawapigia Makofi hii inaletaga maswali mengi sana”

“Lakini huwa tunaweka nia katika mchezo unaofuata kwa sababu Simba ni timu ya watu hatuchezi kama kazi hivyo lazima tulete matokeo wanayoyataka.” alisema Bocco.

Mara kadhaa Mashabiki na Wanachama wa Simba SC wamewapigia makofi wachezaji wao kwa kuwapongeza licha ya kupoteza michezo muhimu ya Ligi Kuu na Michuano ya Kimataifa.

Kitendo hicho Cha Mashabiki na Wanachama kimekuwa kikitafsiriwa kama ukomavu wa kisoka, kufuatia kukubali matokeo na kuwatia moyo wachezaji wao kwa mchezo unaofuata.

Masuala mengine yaliyowekwa wazi na John Bocco ni:

?????????? ?? ?????????? ????? ??

Nilipokuwa Azam nilikuwa nasikia mengi sana ambayo ukiwa mchezaji wa Simba utakutana nayo lakini nilipofika Simba sikukutana na changamoto yoyote ile

Ukiwa mchezaji zipo changamoto unakutana nazo hivyo unazikabili ili uweze kusonga mbele.Simba kuna wachezaji bora sana (sijasema wanaocheza kwingine sio bora) lakini ukiangalia unaweza kuwa mchezaji tishio mfano kwa JKT lakini ukija Simba ukaonekana wa kawaida hii ni kutokana mfano kuna wachezaji wengi wa kigeni hivyo ukiwa mzawa unatakiwa kupambana kuhakikisha unazishinda changamoto zote.

????????? ?? ??????????

Polokwane Fc walivunja makubaliano na mimi.Tuliongea na tukamalizana wakasema ukifika hiki utakikuta na hiki utakikuta lakini nilipofika nikakuta mambo ni tofauti.

??????? ??? ?? ????????

Ishallah Mungu akipenda bado ninayo ndoto ya kucheza nje ya Tanzania.

Simba SC yazuia Fei Toto, Job kuitwa U23
Wanawake kukuza sekta ya nishati